Kaunti  sita pekee zilizo na maabara yakuwahudumia wagonjwa wa Covid19.

Mwenyekiti wa baraza la magavana  nchini aliyepia  gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya amesema kuwa ni kaunti  sita pekee zilizo na maabara yakutosha yakuwahudumia wagonjwa wa Covid19.

Oparanya amesema kaunti hizo ni  Mombasa,Machakos,Wajir,Trans Nzoia,Kilifi na Busia.

Vile vile amesema kuwa zaidi ya wahudumu wa afya  elfu 77 wa kujitolea nyanjani wameajiriwa katika kaunti zote 47  humu nchini ili kusaidia madaktari kupambana na ugonjwa wa Covid19.

Fauka ya hayo ameongeza kuwa kaunti zimepiga hatua katika kutupa mask ambazo zimetumika ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona nakuzipongeza kaunti kwa kupanda miti  ili kufikisha asilimia 10 ya msitu nchini inayotakikana.

Mwandishi Noah Mwachiro