Msimamizi wa Shirika la vijana la Kenya Muslim Youth Alliance kanda ya Pwani Hamis Juma Mwaguzo amelitaka shirika la Feri kuweka mikakati kabambe ili kukabiliana na kuzagaa kwa virusi vya korona.
Mwaguzo amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni feri nyingi zimekumbwa na hitilafu hali inayowafanya abiria kuwa na wasiwasi pindi wanapoabiri ferry.
Ameongeza kuwa ipo haja kwa shirika la ferry kuweka mikakati itakayofuatwa kama njia mojawapo yakuzingatia tahadhari zilizotolewa na idara ya afya ili kuhakikisha kuwa mambukizi ya ugonjwa wa Covid19 yanapungua.
Kauli yake inajiri siku mbili tu baada ya watu 27 kujeruhiwa katika kivuko cha feri wakati feri ya MV likoni na MV kwale zilipongongana na kusababisha mkanyagano wa watu.