Bunge la seneti lapinga uteuzi wa bodi ya kusimamia bustani ya mama ngina

Waziri wa utalii Najib Balala pamoja na bodi mpya ya kusimamia bustani ya Mama Ngina /picha kwa hisani

Na Salim Zani

Bunge la seneti kwa kauli moja limepinga vikali uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari Brown Ondengo kuwa Mwenyekiti wa Bustani la Mamangina hapa Mombasa.

Maseneta hao wakiongozwa na Seneta wa Mombasa Mohammed Faki wameeleza kuwa ni kinaya kikubwa kuona kuwa Waziri wa Utalii kuteua Bodi ya kusimamia Bustani hilo wote wakiwa ni Wageni hakuna mwenyeji wa Mombasa au Pwani kwa Ujumla.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Seneta wa Kwale Issa Boy kuwa haifai raslimali kama hiyo kuongozwa na viongozi walioshika hatamu katika sekta nyengine huku wenyeji wakikosa nafasi kama hizo.

Waziri huyo wa Utalii alimteua Brown Ondengo kuwa Mwenyekiti wa Mamangina siku chache kabla ya kufunguliwa rasmi kwa Bustani hilo kwa Sherehe za Mashujaa zilizongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Ikumbukwe Ondego alikuwa Mkurugenzi wa Bandari ya Mombasa kwa kipindi cha miaka sita kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2005 huku wanchama wengine wa Bodi hiyo wakitoka nje ya Pwani.

Aidha Wawakilishi wadi wa Kaunti ya Mombasa wanatarajiwa kuijadili hoja hiyo ya uteuzi wa Ondego juma lijalo.