Aliyekuwa mwathiriwa wa mihadarati asomea mafunzo ya uendeshaji magari

Said Mwakulomba( katikati )ambaye ni mwathiriwawa dawa za kulevya akikabidhiwa cheti chake cha uendeshaji magari na mkurugenzi wa shirika la Save our Youth (kulia) eneo la Likoni/picha na Mosphine Mukodo

Na Mosphine Mukodo

Huku vijana wengi wakijingiza katika utumizi wa dawa za kulevya  ,wengi wao pia wameweza kujinasua kutokana na utumizi wa dawa hizo.

Hii ni baada ya shirika la kuhamasisha jinsi ya kujinasua kutoka kwa utumizi wa dawa za kulevya la Save our Youth, kutoa mafunzo kwa vijana  wanaotumia mihadarati pamoja na miradi ambayo itawasadia kujiendeleza kimaisha.

Akizunguma katika hafla ya kuwatuza vijana ambao wamejitoa katika utumizi wa dawa za kulevya eneo la Likoni ,mkurungenzi mtendaji wa shirika hilo Hussein Namoya amesema idadi ya vijana zaidi ya 50 ambao walikuwa wameathirika na dawa za kulevya sasa wemeweza kujitoa kwa utumizi huo na wamepokea mafunzo mbalimbali yakiwemo  ya udereva.

Aidha  Namoya ameyataka mashirika mengine  kujitokeza ili kuwasaidia waathiriwa wa mihadarati wakiwemo vijana na wazee ambao ndio tegeme katika jamii.

Hata hivyo Said Mwakulomba ni mmoja wa mwathiriwa ambaye kwa sasa amejinasua kwa utumizi wa dawa za kulevya na amepokea mafunzo ya uendeshaji magari na kupoke.