Wafanyikazi 6000 pwani wapoteza kazi kutokana na kusafirishwa makasha na SGR


Na Mesphine Mukodo na Francis Mwaro
Vugu vugu linalojiita Okoa Mombasa pamoja na madereva wa malori ya kusafirisha mizigo limemshtumu matamshi ya waziri wa utalii Najib Balala ya kuwa makasha ya kusarisha mizogo yanatumika kusafirisha dawa za kulevya
Waziri Balala hapo jana alisema kampuni zinafanya biashra ya usarishishaji na uhifadhi wa makasha CFS hutumika kuhifadhi dawa za kuvyela huku makasha ya mizigo yakitumika kusafirisha miharati hiyo pamoja pembe za ndovu humu nchini.
Hata hivyo mwenyekiti wa vugu vugu hilo Salim Karama amesema matamshi ya waziri Balala ni njia moja ya kupinga msimamo wao wa kuendeleleza maandamo yao ya kupinga agizo la kusafirisha makasha kwa njia ya reli ya kisasa SGR.
Karama amemtaka waziri Balala kukoma kuingilia maswala ya uchukuzi na badala yake kuachila wizara husika huku ikisema idara za serikali ndizo zenye mamlaka ya kuyakagua na kufungua makasha hayo kabla ya kusafirishwa.
Hata hivyo vuguvugu hilo limesema maandamano hayo yataendelea kote nchini wiki ijayo hasa katika maeneo ambayo reli hiyo inapitia .
Wafanyikazi 6000 wameweza kupoteza ajira kutokana na agizo la serikari ya kusafirisha makasha ya mizigokwa njia ya SGR,kampuni 23 ya kusafirisha na kuhifadhi mizigo za CFS zimeweza kufungwa pamoja na malori 15,000 yamesimama kufanya kazi za usafirishaji wa mizigo tangu agizo hilo lilipoanza kutekelezwa.