"> Maandamano ya kupinga kusarifiswa makasha ya mizigo na SGR yapamba moto.

Maandamano ya kupinga kusarifiswa makasha ya mizigo na SGR yapamba moto.

Wafanyabiashara kaunti ya Mombasa waandamana kupinga kusafirishwa kwa makasha ya mizigo kwa njia ya SGR./Picha kwa hisani

Na Geofrey Chiro

Siku mbili  baada ya sherehe za kuiadhimisha Mashujaa kufanyika katika bustani ya MamaNgina kaunti ya Mombasa ,wafanyibiasha pamoja madeva wa matrela wamedelea ma maandano yao kuishinikiza serikali kufutilia mbali agizo la kusafirisha makasha kwa njia ya reli ya kisasa SGR.

Waandamanaji hao wakiongozwa vuguvugu linalojiita okoa Mombasa pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Haki Afrika na Muhuru wanasema wataendela na maandamano hayo kila siku ya Jumatatu hadi pale serikali itakapo sitisha agizo hilo.

Hapo jana vuguguvu hapo jana lilisitisha maandamao yao baada ya kusherehekea siku ya mashujaa na hii leo limeamua kundelea na maandamo hayo ambayo yamesababisha msongamano wa magari katikati mwa jiji la Mombasa.

Hata hivyo waandamanani hao wanamulaumu rais Uhuru Kenyatta kwa kushindwa kulizungumza swala hilo katika hutuba yake ya Mashujaa katika bustani ya Mamangina.

Kulingana na mwenyekiti wa vuguvugu hilo Salim Karama wafanyikazi wengi wameachishwa kazi kutokana na agizo hilo kwa kuwa wamekuwa wakitegemea biashara ya malori.

Wakati huo huo ameiomba serikali kusikiliza kilio chao ili kuwepo na mashindano ya kibiashra baina ya kampuni za kiserikali na zile za kibinafsi kama njia mojawapo ya kuinua uchumi wa pwani.

Salim hata hivyo  amewataka wa pwani kuacha kuhadaiwa na viongozi Kwa misingi ya kisiasa huku akimpongeza Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kwa juhudi zake za kuunga mkono maandamano hayo.