"> Kaunti ya Kilifi ya ongoza kwa ugonjwa wa saratani Pwani

Kaunti ya Kilifi ya ongoza kwa ugonjwa wa saratani Pwani

Na Erick Mbaruk

Huku ulimwengu ukiendelea kuadhimisha mwezi wa saratani kaunti ya Kilifi imetajwa kuongoza kwa vifo vingi vya wagonjwa wa saratani jimbo la Pwani.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Mulika saratani kaunti ya Kilifi takriban asilimia 50 ya wagonjwa wanaougua ugonjwa wa saratani wameaga dunia katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Idadi kubwa ya visa hivi ikitajwa kuchangiwa na aina ya vyakula wanavyokula wananchi.
Florence Kitsao ni mwasisi wa shirika la mulika saratani kaunti ya Kilifi.

Takwimu hizi zikimaanisha kuwa kaunti ya Kilifi inaongoza kwa idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa saratani ukanda wa pwani.

Kulingana na Rebecca Mwandaza ambaye ni muuguzi katika hospitali kuu ya mkoa wa pwani, wagonjwa wengi wanaougua saratani hufika hospitalini kuchelewa ikiwa tayari ugonjwa huo umesambaa katika sehemu kubwa ya mwili.