"> Wakazi Eldoret waandamana kucheleweshwa kwa malipo ya Census

Wakazi Eldoret waandamana kucheleweshwa kwa malipo ya Census

Na Mosphine Mukodo

Miezi miwili baada ya zoezi la kuhesaba watu lifanyike ,baadhiya wafanyikazi ambao walifanya zoezi hilo bado hawajalipwa malipo yao kwa hudumu walizo toa.

Wafanyikazi hao kutoka kaunti ya Uasin Gishu wameandamana mjini Eldoret ili kushinikiza shirika la kitaifa la takwimu la KNBS kuwalipa malipo yao .

Wengi ambao walihusika katika zoezi hilo ni vijana wa shule ,wakidai kuwa wataka pesa hizo ili kulipa karo za shule.

Watu 165,000 waliweza kuajiriwa kwa muda ili kufanya zoezi hilo ambao lilifanya mwezi Agosti huku zoezi hilo likitumi shilingi bilioni 18.5.