"> Mbunge Ken Chonga aitaka serikali kukamisha ujenzi wa chuo cha Ronald Ngala.

Mbunge Ken Chonga aitaka serikali kukamisha ujenzi wa chuo cha Ronald Ngala.

Na Ricks Mbaruk

Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga ameilaumu serikali kwa kuchelewa kukamilisha ujenzi wa chuo cha utalii cha Ronald Ngala eneo la Vipingo kaunti ya Kilifi na kutoa nafasi kwa vijana nchini kusomea utalii ili kushindana katika soko la kimataifa.

Chonga ameilaumu serikali kwa kujikokota kuukamilisha ujenzi wa chuo hicho katika eneo la Vipingo kaunti ya Kilifi chuo kitakacho wawezesha vijana vijana kupata mafunzo ya kuwasadia kupambana kutafuta nafasi za ajira katika uchumi wabaharini.

Amesema chuo hicho kimechukua takriban miaka kumi tangu kuanzishwa kwa ujenzi wake.

Ameisihi serikali kukamilisha ujenzi wa chuo hicho ili kutoa nafasi ya vijana kujiandaa vyema kwa soko la uchumi wa baharini ambalo linakuwa kwa kasi.