"> Kamati ya bunge la sineti yandelea na uchunguzi wa kutimuliwa kwa Samboja.

Kamati ya bunge la sineti yandelea na uchunguzi wa kutimuliwa kwa Samboja.

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta akihutubia waandishi wa habari mjini Voi/Picha kwa hisani

Na Francis Mwaro

Kamati  maalum ya bunge la seneti ambayo imeteuliwa  kuchunguza kutimuliwa madarakani kwa gavana wa kaunti ya Taita Taveta sasa inaendelea na uchunguzi ili kubaini madai ya yalisababisha gavana huyo kutimiliwa na wawakilishi wadi ya kaunti hiyo.

Kamati hiyo ambayo inajumulisha ya watu kumi na moja inaongozwa na seneta wa Embu Njeru Ndwiga ilikutana  jana na leo itawasikiliza mashahidi kutoka  bunge la kaunti ya Taita Taveta ili kukagua nakala muhimu  kuhusiana na kubanduliwa kwa gavana Samboja.

Akizungumza muda mfupi uliopita mwenyekiti wa kamati hiyo Njeru Ndiga amesema pande zote mbili zitapewa nafasi ya kusikilizwa katika uchunguzi wa kutimuliwa kwa Samboja.

Hata hiyo kamati hiyo imelazimika kukatalia mwaliko wa gavana Samboka kufika mbele yake ili kujitetea baada ya mahakama  kusimamisha kamati hiyo kuendelea kusikiliza madai hayo.

Kupitia wakili  wake Nelson Havi   anasema mteja wake hajapatiwa nafasi ya kusikilizwa kabla kubanduliwa na wawakilishi wadi wa bunge hilo .

Wawakilishi wadi wanamulaumu gavana Samboja kwa uongozi mbaya pamoja na kukataa kupitisha bajeti ya kaunti hiyo .

Kamati hiyo iliteuliwa wiki iliyopita ina siku sita kusikiliza madai hayo kabla kuwasilisha ripoti bungeni.