"> Polisi wanzisha uchunguzi wa kifo cha kasisi wa katoliki Likoni.

Polisi wanzisha uchunguzi wa kifo cha kasisi wa katoliki Likoni.

Na Francis Mwaro

Maafisa wa polisi eno la Likoni wameanzisha uchunguzi wa kifo cha kasisi wa kanisa la kikatolika ambaye alipatikana aliaga dunia ndani ya gari lake.

Kulingana na afisa mkuu wa polisi eneo la Likoni Benjamin Rotich, kasisi  Arnest Mutua alipatikana kwenye gari lake ambalo  lililokuwa limeegeshwa karibu na kituo cha polisi usiku wa kuamkia Jumatano akiwa ameaga dunia.

Afisa huyo hata hivo amesemea hakuna ishara zozote za uvamizi japo polisi wanashuku kuwa huenda alikabiliwa na mshtuko wa moyo ikizingatiwa historia inaonyesha kuwa alikuwa akiugua shinikizo la damu mwilini na kisukari

Padri huyo amefariki akiwa na kisukari na alikuwa na umri wa miaka sabiini na tano na amekuwa akihubiri katika kanisa katoliki la infant eneo laMtwapa kaunti ya kilifi kabla ya kifo chake.

Asikofu mkuu wa kanisa  katoliki jimbo la Mombasa Martini Kivuva amethibitisha kifo cha padri Mutua,huku akitarajiwa kuziko Octoba 29.

Kifo cha kasisi huyo kinajiri siku chache baada ya mwili wa kasisi wa kanisa la kikatoliki la Machakos Michael Kyengo kupatikana umeuwawa na kuzikwa katika kaunti ya Embu.

Mwili wa kasisi huyo tayuari umefukuliwa na washukiwa wawili wametiwa mbaroni kufuatia na mauaji ya kasisi huyo.