Rais Kenyatta kuzungumzia swala la SGR kwa kina siku ya Mashujaa

PHOTO: Courtesy

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulizungumzia kwa undani zaidi swala la Kusitishwa kwa makasha yote ya mizigo kusafirishwa kutoka bandarini Mombasa hadi Nairobi kupitia Reli ya kisasa SGR siku ya maadhimisho ya Mashujaa hapa Mombasa.

Mushirikishi wa utawala eneo la Pwani John Elungata amesema kwamba Rais Kenyatta atafafanua zaidi kuhusu swala hilo kwa  wale ambao walikuwa wakitilia shaka tangazo la waziri wa uchukuzi James Macharia kuhusu kusitishwa kwa Mpango huo.