Mradi wa kuwapa sindano watumizi wa mihadarati usitishwe- wanaharakati, Mombasa

PHOTO: Courtesy

Baadhi ya wanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya kanda ya pwani wameyataka mashirika ya kijamii kusitisha mradi wa kutoa sindano kwa watumizi wa dawa za kulevya.

Wanaharakati hao wakiongozwa na Famau Mohammmed Famau, wanasema kuwa licha ya kuwa ugavi wa sindano unalenga kupunguza maambuziki ya magonjwa miongoni mwa waraibu hao,vijana wengi wameingilia kwa uraibu wa dawa za kulevya kutokana na sindano hizo.

Famau amependekeza kubuniwa kwa mbinu mbadala ya kuzuia maambukizi ya magonjwa mbali mbali  miongoni mwa watumizi wa dawa za kulevya badala ya kuwapa sindano ambazo ziko na madhara makubwa katika jamii.

Kauli hii inajiri baada ya eneo la pwani  kuorodheshwa la kwanza  kwa utumizi wa dawa za kulevya huku idadi kubwa wanaotumia dawa hizo wakiwa na vijana wadogo.