Pombe haramu yanaswa na kuharibiwa kaunti ya Bomet

PHOTO: Courtesy

Maafisa wa polisi wamefanikiwa kunasa na kuharibu lita mia mbili ya pombe haramu aina ya changaa eneo la Cheptimtim kaunti ya Bomet.

Katika oparesheni hio iliyoendeshwa mapema hii leo maafisa hao pia wamefanikiwa  kuwatia mbaroni  washukiwa watano wa ugemaji na wauzaji pombe hio huku wakisubiri kufikishwa mahakamani  hii leo.

Constabo spesheli wa polisi Alex Shikondi amedhibitisha hayo na kuwahakikishia wakaazi  wa eneo hilo kuwa msako huo bado  unaendelea .

Aidha  afisa huyo amelalamika kwamba  wanaoathirika na pombe hiyo ni watoto wao kwa hivyo  amewahimiza wakaazi  hao  kushirikiana ili waweze kumaliza utumiaji  na uzaji  wa pombe haramu katika kaunti hiyo.