Wagonjwa wa Saratani wasihi wakenya kuwapa upendo ili kukabiliana na changamoto hiyo

PHOTO: Courtesy

Wagonjwa wa saratani wametoa wito kwa wakenya kusitisha unyanyapaa dhidi yao, wakiongea na waandishi wa habari katika kaunti ya Nakuru, Gladys Wanjiru mwenye umri wa miaka 35 ambaye anaendelea na matibabu baada ya kupatikana na kansa ya matiti mwaka jana, amesema kwamba upendo ni bora kwao katika kukabili changamoto za ugonjwa huo wa saratani.

Mwezi huu wa Oktoba ukiwa ni mwezi ambao unaangazia juhudi ambazo serikali na mashirika mbali mabali yameweza kufanya kukabiliana na ugonjwa wa kansa wanatoa wito kwa wakenya kujitokeza mara kwa mara kufanyiwa vipimo vya kiafya ili iwapo ugonjwa huo utagunduliwa mapema itakuwa rahisi kuukabili.