Kaunti ya Nairobi na Mandera yazitupilia mbali mswada wa punguza mzigo

Mabunge ya kaunti ya Nairobi na mandera yamekuwa ya hivi punde kwenye orodha inayoendelea kupinga mswada wa chama cha Third way Alliance kinachoongozwa na daktari Ekuru Aukot cha mswaada wa punguza mizigo.

Nairobi na mandera zimejiunga na kiambu, nyeri ,Siaya ,Homabay, murang’a Nakuru, makueni na Kirinyaga ambazo tayari zimepinga mswaada huo.

Kiongozi wa wengi kwenye bunge la kaunti ya Mandera Abdi Guyo, ambaye aliwasilisha rasmi mswaada bungeni humo alisema kwamba, iwapo wakilishi wadi wa mandera wangeupitisha mswada huo wangekua wamewasaliti wakaazi wa kaunti hiyo.

Aidha walitoa maoni ya kuupinga kwa kigezo kwamba, baadhi ya vipengele ikiwemo cha kupunguza idadi ya maeneo bunge itawaathiri.