Matiangi achapisha rasmi siku kuu ya Moi day

Photo: Courtesy

Waziri wa usalama wa ndani ya nchi daktari Fred Matiang’i jana alichapisha rasmi kwenye gazeti la serikali kuwa kesho Octoba kumi kuwa siku ya mapumziko kila mwaka nchini.

Hatua hiyo imeafikiwa baada ya mahakama kuu kuagiza siku hiyo, ambayo ilikuwa ikisherehekewa kama siku ya Moi Day baada ya kuondolewa hapo awali kutokana na tafsiri ya katiba.

Wakenya  wametakiwa kuitumia siku hiyo katika maswala mbali mbali ya kijamii pamoja na kuimarisha uzalendo wa nchi.