Watoto wanaougua Anaemia wapewe damu ya kutosha- KEMRI

PHOTO: Courtesy

Taasisi ya Kitaifa cha Utaifati wa Afya KEMRI imebainisha kwamba kupeanwa kwa kiwango kinachofaa cha damu katika matibabu kwa watoto wanaougua maradhi ya anemia kali severe anaemia kutapunguza vifo vya watoto hao.

Takwimu za sasa za Tasisi hiyo zinaonesha kwamba  watoto hao wanahitaji kiwango kikubwa cha damu ikilinganishwa na maelekezo ya sasa ya Shirika la Afya Duniani WHO.

Takwimu hizo zinaonesha kwamba watoto ambao wamepata kiwango cha damu inayohitajika hawako kwenye hatari kubwa ya kufariki dunia ikilinganishwa na ambao wamekuwa wakipata kiwango kidogo cha damu.

Utafiti huo uliofanywa na Profesa Kath Maitland wa KEMRI aidha unaonesha kwamba watoto wanaougua anemia ambayo si kali hawahitaji damu ya  haraka ikiwa tu wanauangalizi wa karibu kwa dalili za anemia kali.

Anemia kali ni maradhi ambayo yamekuwa yakiwaathiri hasa watoto katika maeneo ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Sub-Saharan Africa.