"> Serikali haitatenganisha huduma za Safaricom- Joe Mucheru, Waziri wa mawasiliano

Serikali haitatenganisha huduma za Safaricom- Joe Mucheru, Waziri wa mawasiliano

By Noah Mwachiro

Serikali imesema kuwa haitatekeleza hatua ya kutenganisha huduma za kampuni ya Safaricom, hata baada ya shinikizo kuu kutoka kampuni nyingine za mawasiliano ya simu.

Waziri wa habari na mawasiliano Joe Mucheru amesema hatua ya kutenganisha huduma za kampuni ya Safaricom itawafanya waekezaji kukosa kuwekeza nchini.

Waziri Mucheru alikuwa akizungumza wakati wa kuzindua bodi ya halmashauri ya mawasiliano nchini