"> Serikali yatakiwa kupunguza ushuru wa bidhaa zinazozalishwa nchini

Serikali yatakiwa kupunguza ushuru wa bidhaa zinazozalishwa nchini

Serikali imetakiwa kupunguza ushuru inayotoa kwa bidhaa zinatengezwa humu nchini ili kuambatana na zinatotengezwa kutoka mataifa ya afrika mashariki.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Mombasa,mkurugenzi katika kitengo cha ukuzaji wa biashara katika kampuni ya uzalishaji wa mafuta ya Pwani Oli, Rajul Mandhi, amesema kuwa serikali imekuwa ikitoza wafanyibiashara wa sekta hiyo ushuru mkubwa ikilinganishwa na viwango vya mataifa jirani afrika mashariki.

Aidha Mandhi pia ameitaka serikali kuangazia ada zinazotozwa kwa wafanyibiashara wa Kenya wanaosambaza bidhaa zao katika mataifa ya Afrika mashariki ili wawe katika viwango sawa katika biashara hiyo.

Katika suala la ajenda 4 za maendeleo,Madhi amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuzingatia zaidi sekta ya uzalishaji katika viwanda akidai kuwa ndio sekta muhimu ya kukuza uchumi wa taifa.