"> Wanabiashara walalamika Mombasa

Wanabiashara walalamika Mombasa

                                                Ukarabati wa kueka vigae katika kaunti ya Mombasa

Monje Chai

Wafanya biashara  katika soko kuu la Marikiti  wanalalamikia  upungufu wa wateja katika soko hilo kutokana na shughuli za  ukarabati  wa barabara unaondelea katika  barabara zilizoko katika soko hilo.

Wakiongea na meza yetu ya biashara,wafanyibiashara hao wameelezea kuwa, wengi wa wateja  wanaotembelea soko hilo amekuwa wakighadhabishwa  huku wakiitaka serikali ya kaunti kuendeleza shughuli za ujenzi wakati wa usiku.