"> Wafanya biashara ya malori walalamika kutokana na dhulma Malindi

Wafanya biashara ya malori walalamika kutokana na dhulma Malindi

Lori lillilokamtwa na maafisa wa KENHA likipimwa uzani katika kituo cha kupimwa uzani cha Mariakani/Photo na Erickson Kadzeha.

Wafanya biashara ya uchukuzi wa malori mjini Malindi amelalamikia kukubudhiwa na maafisa wa mamlaka ya kusimamia barabara kuu nchini KENHA.

Wafanya biashara hao wakiongozwa na Caroline Gikunda mweka hazina wa chama cha wamiliki wa malori mjini Malindi cha Transporters of Malindi Sacco Society Limited TRANSMASA wameelezea kuhangaishwa na maafisa hao wakati wa kupima uzani wa mali wanazosafirisha kwa wateja wao.

Amesema maafisa hao hutumia mizani zinazotoa matokeo ya kuzidi kwa uzani unaokubaliwa na sheria za uchukuzi katika barabara kuu tofauti na mizani zinazotumiwa katika vituo vya kupimia uzani vya Mtwapa na Mariakani.

Amesistiza kuwa licha ya chama cha wafanya biashara ya uchukuzi wa malori mjini Malindi kuwa na maelewano na maafisa wa KENHA kuhusu jinsi ya kufanya biashara wafanya biashara hao wamekwa wakihangaishwa na maafisa hao.

Hata hivyo amebaini kusambaratika kwa biashara yao kutokana na maafisa hao kuwaitisha hongo ili kuyaruhusu malori hayo kuendelea kuhudumu katika barabara kuu hizo.

Ameongeza kuwa hali hiyo imechangia benki kunadi zaidi ya malori 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita mjini Malindi kutokana na wamiliki wake kushindwa kulipa mikopo waliyochukuwa kuendeleza biashara hiyo.