"> Afueni kwa wafanyabiasha wadogo wadogo Nairobi

Afueni kwa wafanyabiasha wadogo wadogo Nairobi

Wafanyibishara wadogo  wadogo wanaohudumu katikati mwa jiji la Nairobi  wana kila sababu ya  kutabasamu baada ya ombi lao kupitishwa  na bunge la kaunti hiyo.

Kinyume na hapo awali wafanyibiashra hao  wataendesha biashara zao  bila kutoa kodi ya 25  kila siku.

Afisa mkuu mtendaji wa fedha  kaunti ya Nairobi  Charles  Kerich ameielezea bunge  kuwa hatua  hii itawahusisha hata wale wafanyibiashara ambao wako kando ya  maeneo hayo.

Aidha ameongeza kuwa itasaidia kupata kodi hata kwa wale ambao walikuwa wanakwepa kulipa kila wakati.