"> Shughuli za upakuzi na upakiaji mizigo bandarini Mombasa kuimarika

Shughuli za upakuzi na upakiaji mizigo bandarini Mombasa kuimarika

SHUGHULI za upakuzi na upakiaji wa makasha bandarini Mombasa zinatarajiwa kuimarika zaidi kinyume na hapo awali ambapo kulikuwa kunashuhudiwa msongamano bandarini humo.

Hii ni kufuatia juhudi za serikali kuu kupitia wizara ya uchukuzi nchini kunununua vifaa maalum vya kisasa vinavyotambulika kama Echo Hoppers vitakavyotumika katika shughuli.

Vifaa vya kurahisisha upakuzi na upakiaji wa shehena bandarini-Echo Hoppers. Picha/Wahisani

Afisa wa Mawasiliano katika bandari hiyo Hajj Masemo amesema kuwa vifaa hivyo vinne vilivyoigarimu serikali takriban dola milioni 6.2 za Kimarekani, vilitengenezwa na kampuni ya Samsung Materials Holdings iliyoko nchini Uchina.

Masemo amefichua kuwa vifaa hivyo vitarahisisha shughuli hiyo kwani vina uwezo wa kupakua tani mia saba za mizigo kwa saa moja ikilinganishwa na vifaa vilivyokuwa vikitumika awali ambavyo vilikuwa na uwezo wa kupakua tani mia tatu kwa saa moja.