"> Benki ya Equity yapunguza vuwango vya riba

Benki ya Equity yapunguza vuwango vya riba

Benki ya Equity imetangaza kupunguza viwango vya riba vinavyotozwa mikopo kwa asilimia 14.5 saa chache kabla ya makataa yaliyotolewa na benki kuu ya Kenya kwa benki kupunguza ada zao kukamilika.

Afisa mkuu mtendaji wa equity James Mwangi amesema wateja wa benki hiyo watanufaika pakubwa kufuatia kupunguzwa kwa ada za mikopo huku akitoa wito kwa Wakenya kuchukua nafasi hiyo kuwekeza.

Mwangi vilevile amesema kuwa wateja wote waliowekeza na benki hiyo watakuwa wanapata faida ya asilimia 7.3 kwa viwango vya pesa wanavyoekeza kwa benki hiyo, huku wale walio chukua mikopo kwa benki hiyo wakitakiwa kulipa viwango vya riba asilimia 14.5.

Mwangi aidha amesisitiza kuwa kupunguzwa kwa viwango hivyo kutafanyika kwa mikopo yote inayotolewa na benki hiyo ikiwemo ile ya simu.

Wakati uo huo Mwangi amesema hatua ya benki hiyo imeangazia sheria kwa ukamilifu, kauli iliyoungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa kitaifa katika maswala ya mikopo ya benki hiyo. 

Benki kuu imeonya maafisa wakuu ambao hawatakuwa wameanza kutekeleza sheria hiyo kufikia mwisho wa siku watachukuliwa hatua.