"> Aliyekuwa mkurugenzi wa Safaricom auza hisia zake

Aliyekuwa mkurugenzi wa Safaricom auza hisia zake

Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya safaricom Michael Joseph ameuza nusu ya hisa zake kwa kampuni hiyo huku mrithi wake Bob Collymore akiongeza hisa zake akiwa anaamini mawasiliano ya simu yanaendelea kuongezeka.

Ripoti ya Safaricom ya kila mwaka inaonyesha Joseph kukata umilikaji wake katika kampuni kwa mara ya kwanza tangu orodha yake mwaka 2008 na mauzo ya hisa zaidi ya milioni mbili mwishoni mwa mwezi Machi.

Uamuzi wake wa kuuza sehemu yake mwezi Machi hata hivyo ulimaanisha kwamba amekosa faida huku wawekezaji wakitoa ripoti ya hivi karibuni kuwa bei ya hisa ilipanda kwa shilingi 21.75. na kushuka kwa shilingi 20.75 hapo jana