Bei ya umeme huenda ikapanda

Huenda malipo ya huduma za umeme yakapanda ifikapo mwezi ujao baada ya kiwango cha thuluthi tatu cha nishati kupunguzwa kutoka kwa kituo cha kitaifa.

Kulingana na tume ya kudhibiti kawi nchini marekebisho yanayoendelea katika kituo cha kuzalisha nishati cha Suswa yamesababisha ongezeko hilo baada ya megawati mia 2 za nishati kupunguzwa kutokana na gharama za mafuta na maji yanayozalisha nguvu za umeme.

Hatahivyo mkurugenzi wa tume hiyo Joseph Ng’ang’a amewahakikishia wananchi kuwa hali hiyo ni ya mda hadi watakapodhibiti gharama za umeme nchini katika siku zijazo.

https://yonhelioliskor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287