Nyani azima umeme, KENGEN yasema

Kampuni ya uzalishaji umeme nchini KENGEN  imesema kuwa kupotea kwa nguvu za umeme kote nchini hapo jana kulisababishwa na tumbiri.

Katika taarifa kwa vyombo vya habaro KENGEN imesema kuwa ilimpata tumbiri huyo katika sehemu maalum katika bwawa la Gitaru mashiriki mwa Kenya.

Kampuni ya uzalilishaji na ile ya usambazaji wa nguvu za umeme zimesema kuwa nguvu za umeme zilipotea hapo jana saa tano na nusu na kupelekea kupoteza zaidi ya megawati 180.

Baadhi ya wafanyi biashara humu nchini wamekuwa wakilalamikia kupotea kwa nguvu za umeme kila mara jambo ambalo wanadai kuwa linawasababishia hasara kubwa haswa katika biashara za kimataifa.

 

 

https://boltepse.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287